bunda express yapata ajali jana

Basi la Bunda lililokua linatokea Musoma kwenda Mwanza limepata ajali nje kidogo ya Magu eneo la katikati ya Kahangalala na Ihayabuyaga na watu watatu wanahofiwa kufariki katika ajali hiyo na zaidi ya 10 kujeruhiwa. 

Watoto wakiwa na mama zao wanalia tu wakihitaji msaada, mvua ikiwanyeshea wakihofia usalama wao na mali zao. Hakuna pa kujisitiri kwa watoto hawa ambao walikuwa wakisubiri wazazi wao kuokolewa toka ndani ya basi hilo zaidi ya kujisitiri kwa kanga, vitenge na mashuka waliyoambulia toka kwenye baadhi ya mabegi yao.
Hali ya uokoaji imeathiriwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha eneo hili ni wachache tu abiria wameweza kupewa miamvuli na watu walio kwenye magari yanayopita eneo hili ili wapate kujisitiri
bunda express yapata ajali jana bunda express yapata ajali jana Reviewed by bongo qualities on 4:36 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.