Kwa ufupi
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwamo meneja wa hoteli hiyo, ambaye
alikataa kutaja jina lake hadharani alisema kwamba marehemu huyo
aliwasili hotelini hapo Desemba 3 mwaka huu, saa 1 :00 jioni na kukodi
chumba kimojawapo hotelini hapo.
MFANYABIASHARA wa madini aina ya Tanzanite mkoani Arusha,
Ngerii Olerumwa anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40
amekutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha ndani ya Hoteli ya
Premier Palace ambayo Timu ya Soka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano
imeweka kambi jijini Arusha.
Maiti
ya mfanyabiashara huyo iligundulika saa 3:30 asubuhi jana mara baada ya
mhudumu wa hoteli hiyo kugonga kwa muda mrefu mlango wa chumba
alichokuwa amefikia marehemu huyo bila mafanikio na kisha kubaini
alikuwa amefariki dunia.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwamo meneja wa hoteli hiyo, ambaye
alikataa kutaja jina lake hadharani alisema kwamba marehemu huyo
aliwasili hotelini hapo Desemba 3 mwaka huu, saa 1 :00 jioni na kukodi
chumba kimojawapo hotelini hapo.
Meneja
huyo akisimulia tukio hilo alisema kwamba marehemu aliwasili akiwa peke
yake hotelini hapo na kubainisha kwamba yeye ndiye alikuwa mtu wa
mwisho kukodi chumba hotelini hapo.
Alisema
ilipotimu jana saa 3:30 asubuhi wakati mhudumu wa hoteli hiyo akigonga
mlango wa chumba alichofia marehemu kwa lengo la kufanya usafi mlango
huo haukuweza kufunguliwa kwa wakati hali iliyosababisha kufanya juhudi
za kuufungua mlango huo kwa lazima.
Alisema
kwamba baada ya kufanikiwa kuufungua mlango huo walijaribu kumwamsha
lakini hakuweza kuamka hali iliyowafanya wawaarifu polisi.
Polisi
walifika eneo la tukio na kuchukua maelezo kwa baadhi ya watumishi wa
hoteli hiyo wakiwamo walinzi wa hoteli hiyo huku baadhi ya wabunge
wanaounda timu ya wabunge wakitaharuki kutokana na tukio hilo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti ndugu wa marehemu ambao walikusanyana nje ya hoteli
hiyo walisema kwamba wameshtushwa na kifo cha ndugu yao na wanahisi
kwamba aliuawa katika mazingira ya kutatanisha huku wakiwataka polisi
kubaini chanzo cha kifo cha marehemu.
Akihojiwa
na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabass
alikiri kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza kwamba uchunguzi
unaendelea.
Sabas alisema kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ndani ya Hospitali ya Mkoa ya Mt. Meru na atatoa taarifa kamili ya tukio hilo kuanzia leo mbele ya waandishi wa habari.

Mfanyabiashara afia hoteli ilimopanga Timu ya Bunge
Reviewed by bongo qualities
on
8:13 AM
Rating: