Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (wapili kulia) akiambatana na wafuasi wa Chadema wakitoka nje ya Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam jana, baada ya kusikilizwa rufaa yake ya kupinga kuvuliwa ubunge wake
Kwa ufupi
Lema
alivuliwa ubunge April 5, 2012, katika hukumu iliyotolewa na Jaji
Gabriel Rwakibalia, kufuatia kesi iliuyofunguliwa makada watatu wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel,
wakipinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
WAKILI wa Serikali Mkuu Timon amedai kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ilikosea kutengua ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, kwa madai ya kutumia lugha za matusi kwa kuwa Bunge limeruhusu wanasiasa kutukanana kwenye kampeni.
Wakili
Vitalis alitoa madai hayo jana, wakati wa usikilizwaji wa rufaa ya
Lema, aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema),katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam.
Wakati
wakili huyo wa serikali akitoa madai hayo, Wakili wa wajibu rufaa,
ambao walishinda katika kesi ya msingi, Alute Mughway, naye alidai kuwa
Mahakama Kuu, Arusha ilikosea katika uamuzi wake, pamoja na mambo
mengine, kwa kukataa baadhi ya madai yao.
Lema
alivuliwa ubunge April 5, 2012, katika hukumu iliyotolewa na Jaji
Gabriel Rwakibalia, kufuatia kesi iliuyofunguliwa makada watatu wa
Chama cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel,
wakipinga ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Lema
kupitia kwa Wakili wake Method Kimomogoro alikata rufaa Mahakama ya
Rufani, lakini Novemba 8, 2012 mahakama ilitupilia mbali rufaa hiyo
baada ya kuini kuwepo kwa dosari za kisheria, kutokana na pingamizi
lililowekwa na upande wa wajibu rufaa.
Hata
hivyo mahakama hiyo ilimpa nafasi nyingine ya kukata rufaa tena baada
ya kumpa siku 14 kufanya marekebisho ya dosari hizo za kisheria na
kuiwasilisha mahakamani ndani ya muda huo, amri ambayo aliitekeleaza.
Wakati
Lema akikata rufaa kupinga hukumu ya Mahakama Kuu kumvua ubunge, wajibu
rufaa nao walikata rufaa (Cross Appeal) kupinga uamuzi wa mahakama
hiyo, huku wakibainisha hoja nne.
Katika
hoja ya kwanza hadi ya tatu walidai kuwa Jaji alikosea katika hukumu
yake kwa kuchanganya vituo vilivyotolewa ushahidi na mashahidi wanne na
hatimaye akakataa ushahidi wapo, pamoja na tarehe za ratiba ya kampeni
ya CCM nay a Chadema.
Hoja
ya nne walidai kuwa Jaji alikosea kwa kuamua kuwa hata kama Lema kwenye
kampeni zake alidai kuwa Dk. Buriani ni mkazi wa Zanzibar hatafaa,
wakidai kuwa ukazi si sifa ya kuchaguliwa kuwa mbunge.
Hatimaye
rufaa hizo zilisikilizwa jana na jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya
Rufani, lililoundwa na Jaji Salum Massati, Jaji Bernard Luanda, chini
ya uongozi wa Jaji Nathalia Kimaro.
Wakati
wa usikilizwaji wa rufaa hiyo, mawakili wawili ambao ni ndugu, Mbunge
wa Singida Mashariki, Tundu Lisu na kaka yake Mghway, walipambana
vikali kwa hoja za kisheria.
Lisu,
Kada wa Chadema ambaye pia ni Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Bungeni, alikuwa akimtetea Lema mrufani (Lema), akisaidiana na Wakili
Method Kimomogolo, huku Mughway akiwatetea wajibu rufani ambao ni
makada wa CCM.
