Tanzania yashinda Vivutio Vitatu Maajabu Saba ya Asili Afrika, ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya Serengeti
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akipiga makofi mara baada ya kumkabidhi tuzo
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi anayenyanyua juu
juu tuzo ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mara baada ya kuitangaza mbuga
hiyo kuwa ni moja ya maajabu saba ya asili katika bara la Afrika kwenye
hoteli ya Mount Meru, Kushoto ni Bw Philip Imler Mwanzilishi wa Taasisi
ya Seven Natural Wonders Bw. Philip Imler.
Tanzania
imefanikiwa kushinda kupitia vivutio vyake vitatu vya utalii ambavyo ni
Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya wanyama ya Serengeti,
hafla hiyo imehudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na
Mabalozi, Wafanya biashara,Mawaziri, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania na wadau mbalimbali wa utalii kutoka Mataifa
mbalimbali katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika
picha kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki na
Lynn Imler mmja wa wakurugenzi wa Taasisi ya Seven Natural Wonders.

Waziri
Mkuu Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya picha ya Ngorongoro Crates
muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders
Bw.Phillip Imler mara baada ya kumalizika kwa hafla ya kutangaza maajabu
saba ya asili ya Afrika iliyofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini
Arusha.
Vikundi wa ngoma kutoka makabila ya mkoa wa Arusha vilipamba hafla hiyo kama vinavyoonekana.
.
Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania wakiwa katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa dini walihudhuria pia
Mwanamuziki Mrisho Mpoto na Kundi lake wakitumbuiza wakati wa utoaji wa tuzo hizo.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Bodi ya Utalii Bi Devitha Mdachi akiwa pamoja na maafisa
wengine wa bodi hiyo wakipokea wageni mbalimbali waliofika katika hafla
hiyo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza jambo na
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Maimuna Tarishi katikati ni msaidizi wake Bw.
Miskanji.
Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Waziri
Mkuu akiwa meza kuu pamoja na viongozi wengine wakati wa utoaji wa tuzo
hizo za Seven Natural Wonders jijini Arusha jana jioni., kutoka kulia
ni Magesa Mulongo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Agness Agunyu Waziri wa Utalii
kutoka nchini Uganda na kutoka kushoto ni Bw. Philip Imler kutoka
Taasisi ya Seven Natural Wonders na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi
Khamis Kagasheki.
Mkurugenzi
wa Hifadhi za taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiwasikiliza wabunge
waliohudhuria katika hafla hiyo kulia ni Deo Filikunjombe na kushoto ni
David Kafulila.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na mbunge wa
jimbo la Arusha Mjini Bw. Godbless Lema kabla ya kuanza kwa hafla
hiyo.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki akiongea katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa TANAPA Bw. Allan Kijazi akiongea katika hafla hiyo.
Muanzilishi na muandaaji wa shindano la Seven Naturaral Wonders Bw.Phillip Imler akizungumza katika hafla hiyo.
Tuzo ya mlima Kilimanjaro ikapokelewa na mhifadhi wa mlima huo kulia ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Philip Imler kushoto.
![]() | |
Add caption |
Balozi
Khamis Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii
akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Mount
Meru jijini Arusha.
Waziri Mkuu
Balozi
wa Kenya nchini Tanzania akizungumza na Balozi Charles Sanga Mwenyekiti
wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB na Mkurugenzi wa bodi hiyo Dk.
Aloyce Nzuki wakati wa hafla hiyo.
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
TANZANIA
imepata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika kupitia vivutio vyake bora
vya utalii vya Mlima Kilimanjaro,Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya
Serengeti ambayo ndio iliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko nchi
nyingine yeyote.
Akitangaza
matokeo hayo jana mjini hapa rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk.
Phillip Imler wa Marekani mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda alisema
sababu iliyopelekea Tanzania kupata ushindi huo ni kutokana na kuwa na
vivutio vya kipekee.
Akielezea
hifadhi ya taifa ya Serengeti alisema kuwa ndio hifadhi ya kipekee
iliyopata kura nyingi na kutokana na tabia za misafara ya wanyama
wanaohama kwa msimu maarufu kama annul animal migration.
Waziri
Mkuu Mizengo Pinda, aliyekuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo, alisema
kuwa nchi za Afrika zina vivutio vingi vya utalii na fursa kubwa ya
kukuza pato kupitia utalii huo.
Alisema
kutokana na sifa ambayo Tanzania imezipata kupitia vivutio vyake vitatu
itaendelea kuvitunza kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na
kuongeza pato la taifa.
“Afrika
ina vivutio vingi vyenye kuvutia hivyo kila nchi ni lazima ijivunie
rasilimali hizo kwa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema
“Kwa
Tanzania ni bahati ya pekee kwa kuweza kupata tuzo tatu za maajabu saba
ya Afrika ambazo ni za Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro pamoja na
hifadhi ya Taifa ya Serengeti hivyo ni wajibu wa kuvitunza na
kuviendeleza,”alisema Pinda.
Aliongezea
kuwa iwapo watanzania wataendeleza tabia ya utunzaji wa vivutio
vilivyopo nchini, nchi itaendelea kupata sifa duniani kote.
Naye
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Dkt. Alan Kijazi alisema mlima
Kilimanjaro ni mlima mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya
kushinda na watanzania waendelee kuutunza.
Dkt
Kijazi alisema kuwa hifadhi hiyo imeshinda kwa kuwa kuwa na wanyama wa
kila aina kama Big Seven, Simba, tembo, Viboko, Nyati, Vifaru, Sokwe na
Mamba.
Mbali
na Tanzania Dk.Imler alivitaja vivutio vingine vilivyoshinda kuwa ni
Red sea Reefs, Okavango Inland delta iliyopo nchini Botwasana, Sahara
Desert na River Nile.
Aidha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema ushindi
huo ni historia kubwa duniani na kwamba ni jambo la watanzania wote
kujivunia.
Pia aliwashukuru wananchi walioshiriki katika mchakato mzima wa kupiga kura na kuviwezesha kuingia katika ushindi kwa mara tatu.
Tanzania yashinda Vivutio Vitatu Maajabu Saba ya Asili Afrika, ni Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crates na Mbuga ya Serengeti
Reviewed by bongo qualities
on
9:35 PM
Rating:
