WAKAZI wa Tarafa ya Lupembe, Mkoa wa
Njombe wamesema wanataka Katiba mpya itamke viongozi ambao watatambulika
kuwa mafisadi, wapewe adhabu ya kunyongwa.
Licha ya pendekezo hilo, walisema wanataka watu
watakaobainika kuwapa wanafunzi wa kike mimba, wapewe adhabu ya kufungwa
jela miaka 30 na kuchapwa bakora 12 wakati wakuingia jela na kutoka.
Wakitoa maoni yao juzi kwa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, walisema mtu akiwa fisadi ni wazi anataka kuwaua wananchi kwa
kuwafanya waendelee kuwa maskini.
Alfred Sanga (50), alisema kiongozi akiwa fisadi ni wazi anataka kuwaua wananchi kwani anasababisha wakose mahitaji yao muhimu ya binadamu.
Alfred Sanga (50), alisema kiongozi akiwa fisadi ni wazi anataka kuwaua wananchi kwani anasababisha wakose mahitaji yao muhimu ya binadamu.
Sanga alisema wananchi wengi wanalalamika maisha
magumu kwa kukosa fedha, lakini baadhi ya watu wanahujumu uchumi kwa
kujilimbikizia mali jambo ambalo siyo jema.
“Nataka Katiba mpya iseme kwamba kiongozi fisadi
atapewa adhabu ya kunyongwa, kwani huyo hawatakii mema wananchi,”
alisema Sanga na kuongeza:
“Haiwezekani wananchi kila siku wanapiga kelele
maisha magumu, halafu watu wachache wanajinufaisha wenywe kwa kumiliki
majumba ya kifahari, magari, kutibiwa nje ya nchi na kusomesha watoto
wao nje.”
Sanga alibainisha kwamba hakuna mwananchi
asiyependa kuishi maisha mazuri na kwamba, kitendo cha mtu mmoja
kusababisha wengine kuwa maskini ni sawa na uhaini.
Naye Daud Mgaya (48), alisema mafisadi hawapaswi
kupewa adhabu ya kusimamishwa kazi na kuhamisha vituo vya kazi, bali
kunyogwa kwa makosa ya kuhujumu uchumi na kutaka kuwaua wananchi kwa
umaskini.
“Nashangazwa na kitendo cha fisadi kuundiwa tume
ya kuchuguzwa, kwani huko ni kumaliza fedha za Watanzania bila sababu
za msingi,” alisema Mgaya na kuongeza:
“Naomba Katiba mpya itamke kwamba mtu akibainika kuwa fisadi hatapewa adhabu ya kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi, wala kuundiwa tume ya uchunguzi, au kuhamishwa kito cha kazi.”
“Naomba Katiba mpya itamke kwamba mtu akibainika kuwa fisadi hatapewa adhabu ya kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi, wala kuundiwa tume ya uchunguzi, au kuhamishwa kito cha kazi.”
Badala yake, Mgaya alisema fisadi apewe adhabu ya
kunyongwa ili asionekani tena kulingana na kosa lake kufanana na
mauaji, kwani kula fedha za wananchi ni kutaka wafe na njaa.
Wapendekeza mafisadi nchini wanyongwe
Reviewed by bongo qualities
on
2:28 PM
Rating: